Wiki kadhaa nyuma alichaguliwa kuwa kocha mpya wa klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza la nchini Uingereza, Derby County na siku kadhaa zijazo atatimiza miaka 40 toka kuzaliwa kwake pale nchini Uingereza lakini leo ni kumbukumbu yake ya kusajiliwa kwa Chelsea kwa mara ya kwanza akitokea klabu ya West Ham ya nchini London kwa paundi milioni 11.
Nadhani ushamfahamu na ushaelewa ni nani namzungumzia hapa. Ni mfungaji bora wa muda wote pale klabuni Chelsea, Frank Lampard. Kama nilivyokwambia leo ni kumbukumbu ya siku yake ya kwanza kusajiliwa na Chelsea akitokea West Ham klabu iliyomkuza na klabu iliyokuwa na maana kubwa kwake haswa kutokana na baba yake mzee Frank Lampard Sr kuwai kuichezea na kuifundisha klabu hiyo.
Tarehe 14-Juni-2001, ndiyo siku usajili huo ulikamilika na sababu kubwa inayotajwa kumfanya kutua Chelsea ilikuwa ni maelewano mabovu kati ya klabu hiyo ya West Ham pamoja na kocha wake mkuu kipindi iko, Harry Redknapp ambaye ni mjomba wa Frank Lampard. Ndiyo ni Redknapp huyuhuyu unayemfahamu aliyetamba na klabu ya Tottenham, ana undugu na Lampard na kuondoka kwake West Ham kukamfanya pia baba wa Lampard aliyekuwa moja ya watu wa benchi la ufundi kuamua kuondoka klabuni hapo na kumfanya pia Frank Lampard mwenyewe kuondoka na kuamua kutimkia Chelsea ambayo ilimnasa kwa paundi milioni 11.
Kutua kwake Chelsea kulikuwa na maana kubwa sana kwake haswa kurokana na kujenga historia kubwa sana klabuni hapo akiweza kufunga magoli kibao mpaka kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi kwa muda wote klabuni hapo lakini akiisaidia kushinda mataji kibao akiichezea kwa miaka 13.
Ligi ya mabingwa barani Ulaya, Ligi kuu Uingereza na mataji mengine kibao ameshayashinda akiwa kama mchezaji wa Chelsea.
Nakumbuka vyema aliporejea Stamford Bridge mara baada ya kustaafu soka ambapo hakupata nafasi ya kuongea maneno mengi lakini alirejea kusema asante kwa mashabiki wa Chelsea ambapo moja ya maneno aliyoyasema alisema ipo siku atarejea kutoa asante yake akiwa kama kocha na kwa kuwa sasa ameanza rasmi majukumu ya ukocha naamini ipo siku ataitwa kocha wa Chelsea.
No comments:
Post a Comment