Arsenal wamtaka Luiz, lakini Chelsea wana mpango mwengine kabisa kwake - Darajani 1905

Arsenal wamtaka Luiz, lakini Chelsea wana mpango mwengine kabisa kwake

Share This

Nyota wa Chelsea, David Luiz amecheza michezo 17 tu msimu uliopita wakati msimu mmoja kabla alihusika kwenye kuisaidia Chelsea kushinda taji la ligi kuu Uingereza. Alicheza na kuhusika karibu kwenye kila mchezo. Lakini majeraha yamemfanya kuwa nje kwa muda mrefu msimu huu  ingawa kumekuwa na fununu au uzushi kwamba sababu iliyomfanya kutokupata nafasi ni kutokana na kutofautiana na kocha wake wa Chelsea, Antonio Conte.

Gazeti la nchini Ufaransa, Le 10 Sport limetoa ripoti likisema mlinzi huyo raia wa Brazil amewekewa ofa ya paundi milioni 17 ili ajiunge na klabu ya Arsenal lakini Chelsea inatajwa kukataa ofa hiyo.

Arsenal wanatajwa kumfukuzia mbrazil huyo lakini ofa yao ya kwanza imekataliwa na Chelsea inatajwa kuwa na mpango mwengine kwa mlinzi huyo, ni mpango gani ambao Chelsea inayo kwa nyota huyo mwenye miaka 31.

Inaelezwa kwamba Chelsea inataka kumtumia Luiz kama sehemu ya ofa ya kumnasa kocha Maurizio Sarri kutoka Napoli ingawa ofa hiyo inaambaambaa.

No comments:

Post a Comment