Chelsea na Liverpool kufanya biashara - Darajani 1905

Chelsea na Liverpool kufanya biashara

Share This

Chelsea inatajwa kukaribia kukubali dili la kumuuza mlinda mlango wake nambari moja kikosini hapo, Thibaut Courtois ambaye kwa sasa yupo kwenye majukumu yake ya kuiongoza timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Urusi.

Mlinda mlango huyo mwenye miaka 26 amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake wa kusalia klabuni Chelsea, hali inayoifanya Chelsea kutamani kumuuza ili ipate donge nono kuliko mkataba huo kumalizika na nyota huyo kuondoka bure huku kukiwa na taarifa za nyota huyo kukataa kusaini mkataba mpya lakini pia ikielezwa kama kusaini mkataba mpya wa  kusalia 'The Blues' anataka afanye hivyo mpaka kumalizika kwa Kombe la Dunia na Chelsea ipo tayari kumpa mkataba wenye ofa ya mshahara utakaomfanya kuwa mlinda mlango anayelipwa zaidi.

Lakini kuna taarifa zinadai Chelsea inaweza kukubali ofa kutoka klabu ya Liverpool ambao wanatajwa kumfukuzia mlinda mlango huyo lakini kama wakimkosa Allison Becker kutoka AS Roma ambaye anafukuziwa pia na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment