Chelsea yakamilisha malipo ya Kepa - Darajani 1905

Chelsea yakamilisha malipo ya Kepa

Share This

Mlinda mlango raia wa Hispania, Kepa Arrizabalaga anakaribia kutua Chelsea mara baada ya klabu anayoichezea kuthibitisha kwamba Chelsea imekubali kulipa fungu linalotakiwa kulipwa ili kusajiliwa kwa kipa huyo.

Dau ililotakiwa kutolewa ili kumnasa kipa huyo mwenye miaka 23 lilikuwa ni paundi milioni 71 na inaelezwa kwamba Chelsea imeshakamilisha malipo ya mhispania huyo anayekaribia kukamilisha vipimo vyake vya afya ili atue Chelsea.

Kusajiliwa kwa Arrizabalaga kunamaanisha kwamba mlinda mlango Thibaut Courtois anakaribia pia kusaini kujiunga na klabu ya Real Madrid.

No comments:

Post a Comment