Chelsea yatoa kifua mbele huku Hazard na Kante wakiwemo uwanjani - Darajani 1905

Chelsea yatoa kifua mbele huku Hazard na Kante wakiwemo uwanjani

Share This

Klabu ya Chelsea inafanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wa mwisho wa kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019 mara baada ya kupata ushindi wa magoli 5-4 katika hatua ya matuta dhidi ya klabu ya nchini Ufaransa, Olympique Lyon.

Mchezo huo ambao uliisha dakika 90' za mchezo kwa sare tasa ya 0-0 huku kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri akikifanyia mabadiliko kikosi chote kilichoanza na kuwaingiza wachezaji wengine 11 wakiwemo Eden Hazard, N'Golo Kante, Olivier Giroud na mlinda mlango nambari tatu, Robert Green ambaye alikuwa chachu ya ushindi huo mara baada ya kuokoa penati ya mwisho kwa Olympique Lyon kabla ya Eden Hazard kupiga penati ya ushindi kwa Chelsea..

Mchezo huo unamaanisha Chelsea inacheza ikiwa chini ya kocha Maurizio Sarri michezo minne mfululizo huku ikishindwa kuondoka na ushindi katika muda wa kawaida wa dakika 90'

Mchezo unaofata
Huddersfield Town vs Chelsea
Tarehe 11-Agosti
Saa 17:00 (EAT)
Uwanja: Kirkless Stadium-Uingereza

No comments:

Post a Comment