M/Kirafiki; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Lyon - Darajani 1905

M/Kirafiki; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Lyon

Share This

Chelsea inashuka uwanjani usiku huu wa leo ili kucheza mchezo wake wa mwisho wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu huku ikicheza karika mfululizo wa michezo ya Kombe la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup-ICC)

Kuelekea kwenye mchezo huo hapa nakuletea taarifa na mambo ya muhimu unayopaswa kuyajua kuhusu mchezo huo unaochezwa uwanjani Stamford Bridge huko London nchini Uingereza.

Chelsea;
Nyota wote wa Chelsea wameshaanza mazoezi kasoro mlinda mlango nambari moja, Thibaut Courtois ambaye amegoma kuripoti klabuni ili kushinikiza uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Eden Hazard, N'Golo Kante, Olivier Giroud wote wamesharejea nasasa Chelsea inaonekana kuwa kamili kucheza mchezo wake hii leo.

Olympique Lyon
Nabil Fekir bado hajathibitishwa kama atacheza mchezo huu wa leo haswa kutokana na kurejea mazoezini jana jumatatu.

Rekodi;
Chelsea haijawai kukutana dhidi ya Olympique Lyon hivyo kuufanya mchezo huu kuwa wa kwanza klabu hizo kuwai kukutana.

Muda: Saa 10:05 Usiku (Saa 22:05) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment