Rasmi; Nyota mwengine wa Chelsea akamilisha uhamisho wake - Darajani 1905

Rasmi; Nyota mwengine wa Chelsea akamilisha uhamisho wake

Share This
Kupitia tovuti ya Chelsea, imeripoti kumtoa kwa mkopo mchezaji wake raia wa Jamhuri ya Czech, Tomas Kalas ambaye amejiunga kwa mkopo na klabu ya Bristol city ya nchini Uingereza.

Nyota huyo anayecheza nafasi ya ulinzi aliichezea klabu ya Fulham kwa mkopo msimu uliopita na kuisaidia kufudhu kucheza ligi kuu Uingereza


Alipohojiwa muda mfupi mara baada ya kujiunga na Bristol city, nyota huyo alisema "Nina furaha kuwa hapa, nina furaha kujiunga na timu inayopenda kucheza soka na yenye historia kubwa"

Kalas anatimiza idadi ya wachezaji 32 kutolewa kwa mkopo na Chelsea na amejiunga kwenye klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championships.

No comments:

Post a Comment