Nyota wa Chelsea ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji klabuni hapo, Tammy Abraham anahusishwa kukaribia kuondoka kwa mkopo klabuni hapo.
Tammy Abraham ambaye msimu uliopita alitumika kwa mkopo akiwa na klabu ya.Swansea ya nchini Uingereza anahusishwa kwa karibu kujiunga na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championships.
Lakini wakati huohuo imetoka taarifa inayodai kwamba klabu ya Tottenham Hotspurs ilijaribu kumsajili nyota huyo ambaye ni zao la akademi ya Chelsea lakini Chelsea ikagoma kumuuza. Inaelezwa kwamba klabu hiyo ya Tottenham ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 25 ili kumsajili siku ya mwisho ya dirisha la usajili kufungwa lakini Chelsea ikagoma
kumuuza.
No comments:
Post a Comment