Hazard achukizwa kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Hazard achukizwa kuondoka Chelsea

Share This

Chelsea imefanikiwa kushinda michezo yake minne ya kwanza ya ligi kuu Uingereza na kufanikiwa kufikisha alama 12 katika msimamo wa ligi kuu uku ikishika nafasi ya pili katika msimamo huo ikiachwa nyuma na Liverpool ambao wao wana alama 12 lakini wana faida ya magoli ya kufungwa na kufunga wakiwa na tofauti ya goli moja na Chelsea.

Lakini wiki hii hakutokuwa na mwendelezo wa michuano hiyo ya ligi kuu ambapo itasimama ili kupisha michezo ya kimataifa ambapo baadhi ya wachezaji wataungana na timu zao za taifa ili kucheza michezo hiyo inayotambulika na chama cha soka duniani (FIFA).

Lakini jambo hilo la kusimama kwa ligi hiyo halionekani kuwa zuri kwa nyota na winga wa Chelsea, Eden Hazard ambaye anasema alikuwa anatamani aendelee kubaki na kikosi chake cha Chelsea ili azidi kuisaidia kushinda michezo na kujiweka sawa kwenye kupambania kwake kutwaa ubingwa wa ligi kuu na michuano mingine akiwa na Chelsea.

"Nadhani kwasasa tupo sawa, tunashinda michezo yetu. Nadhani tunacheza mpira mzuri, kwahiyo nafurahia na ninajisikia vizuri"

"Natakiwa niendelee kuwa bora kama nilivyo kwasasa. Jambo ambalo limenihudhunisha ni kwamba kwasasa tunaenda kujiunga na timu zetu za taifa, nilikuwa natamani niendelee kuwa pamoja na wenzangu tucheze wote klabuni Chelsea na tuendelee kupata ushindi" alisema Hazard.

Hazard mpaka sasa kwenye michezo minne ya ligi kuu amefanikiwa kuhusika moja kwa moja katika magoli manne akifunga mawili na kutoa pasi mbili za mabao.

Chelsea itacheza mchezo wake unaofata wa ligi kuu Uingereza dhidi ya klabu ya Cardiff city siku ya tarehe 15-Septemba kwenye uwanja wake wa Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment