Sikia alichokisema Neymar kuhusu usajili wake wa kutua Chelsea - Darajani 1905

Sikia alichokisema Neymar kuhusu usajili wake wa kutua Chelsea

Share This

Dau la paundi milioni 198 alilosajiliwa akitokea Barcelona na kutua PSG linamfanya 
Neymar Jr kuwa mchezaji ghali zaidi duniani kuwai kusajiliwa na sasa kuna taarifa mpya imeripotiwa na moja ya magazeti na tovuti ya habari za michezo barani Ulaya ikimuhusisha nyota huyo raia wa Brazil na klabu ya Chelsea

Taarifa hiyo inasema kwamba klabu ya Chelsea pamoja na klabu ya Arsenal zina nafasi kubwa ya kumnasa nyota huyo.

Taarifa hiyo iliyoripotiwa kutoka kwa mahojiano yaliyofanyika na moja ya watu wake wa karibu ambapo alipohojiwa alisema kwamba nyota huyo yupo tayari kujiunga na ligi kuu Uingereza lakini kwa klabu zinazopatikana kwenye jiji la London.

"Mara kadhaa amekuwa akitembelea jiji la London na amekuwa akivutiwa na kufurahi kila anapofika London" kilisema chanzo hicho.

Na kusema kwamba nyota huyo anavutiwa na ligi kuu Uingereza na huenda akajiunga na moja ya klabu zinazopatikana kwenye jiji la London ikiwemo klabu ya Chelsea inayopatikana kwenye jiji hilo.

No comments:

Post a Comment