Musonda ageuka gumzo mtandaoni - Darajani 1905

Musonda ageuka gumzo mtandaoni

Share This
Kabla ya hapo kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya ambalo lilifungwa siku ya tarehe 31-Agosti, nyota na winga wa Chelsea, Charly Musonda Jr alikamilisha uhamisho wake wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Vitesse ya nchini Uholanzi.

Lakini uhamisho huo umeonekana kutopokelewa kwa furaha kwa winga huyo raia wa Ubelgiji ambapo kupitia mtandao wa Instagram, amefura picha zake zote na kuacha kuifatilia (unfollow) klabu yake ya Chelsea pamoja na wachezaji wa klabu ya Chelsea.

Hii inatafsiriwa kama mwanzo mpya kwake kutaka kuachana na Chelsea jumla ambapo huenda kutokupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea kunamkera na kutaka kuachana na klabu hiyo.

Kwasasa nyota huyo mwenye asili ya Zambia ambaye ana miaka 21 ana mkataba na Chelsea unaomalizika mwaka 2022.

UCHAMBUZI:
Haya ndo madhara ya wachezaji vijana. Inaonekana hapendezewi na anavyokosa nafasi kwenye kikosi cha wakubwa wakati kuna wenzake akina Victor Moses walitolewa kwa mkopo kwenye klabu tatu lakini bado akazidi kusema anatamani kuendelea kutafuta namba Chelsea. Ni utoto mwingi na kusifiwa sana kwamba anajua basi kashajiona ni mchezaji mkubwa.

No comments:

Post a Comment