Ni siku nyengine tamu kwa kila mpenzi na shabiki wa Chelsea mara baada ya klabu yetu pendwa ya Chelsea kufanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya klabu ya Bournemouth ambayo ilikuwa ugenini.
Mchezo ulianza uku Chelsea ikimikiki mpira kwa kiasi kikubwa ikiwa na mfumo wake mpya kutoka kwa kocha Maurizio Sarri ambapo imekuwa ikicheza mfumo.wa 4-3-3 lakini ikitumia zaidi pasi fupi
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa sare ya 0-0 uku Chelsea akiutawala mchezo kwa kiasi kikubwa lakini pia nyota wa Chelsea akipewa kadi ya njano katika kipindi iko cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza uku kocha Maurizio Sarri akiingiza timu bila kufanya mabadiliko ya wachezaji mpaka ilipofika dakika ya 61' ya mchezo ambapo alimtoa Alvaro Morata na kumwingiza Olivier Giroud kabla ya dakika chache baadae kumtoa Willian na kumwingiza Pedro Rodriguez ambapo mabadiliko hayo yalionyesha kuwa na faida mara baada ya dakika chache zikitumika kumfanya Pedro Rodriguez kufunga goli la kwanza akipokea pasi kutoka kwa Giroud.
Wakati Chelsea ikionekana kuendelea kumiliki mchezo huo na kutengeneza mashambulizi zaidi, dakika ya 81' nyota wa Chelsea, Eden Hazard akafanikiwa kuifanya Chelsea ipate uongozi wa goli la pili uku ikifanikiwa pia kupata ushindi huo muhimu kwa Chelsea.
Kwa matokeo haya yanaifanya Chelsea kufikisha alama 12 katika michezo yake minne yaani ushindi wa nne katika michezo minne ya ligi kuu Uingereza.
Rekodi zilizowekwa;
1. Mlinzi na nyota wa Chelsea, Antonio Rudiger amefanikiwa kuichezea mchezo wa 50 klabu ya Chelsea toka aliposajiliwa akitokea klabu ya AS Roma ya nchini Italia mwaka 2017.
2. Kocha Maurizio Sarri amefanikiwa kuingia katika orodha ya makocha sita waliowai kushinda michezo minne ya mwanzo katika ligi kuu Uingereza

No comments:
Post a Comment