Ligi kuu Uingereza: Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Bournemouth - Darajani 1905

Ligi kuu Uingereza: Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Bournemouth

Share This
Chelsea inashuka uwanjani jioni ya leo ili kucheza mchezo wake wa nne wa ligi kuu Uingereza ambapo itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Bournemouth ambao wana kumbukumbu nzuri katika mchezo wa mwisho uliochezwa Stamford Bridge uliisha kwa Chelsea kupoteza kwa magoli 0-3

Hapa nakuletea habari muhimu unazopaswa kuzijua kuhusu mchezo huo ambao utatumia vumbi pale Darajani.

Chelsea:
Cesc Fabregas anaendelea kukosekana kutokana na majeraha aliyokuwa nayo ingawa kocha Maurizio Sarri amesema nyota huyo hana majeraha makubwa. Tammy Abraham amejiunga kwa mkopo na klabu ya Aston Villa ambapo kuondoka kwake kunaifanya Chelsea ibaki na washambuliaji wakati wawili Alvaro Morata na Olivier Giroud

Mwamuzi:
Mwamuzi Lee Mason mwenye umri wa miaka 46 mzaliwa wa Bolton nchini Uingereza amechaguliwa kuwa mwamuzi katika mchezo unaokuja wakati Chelsea itakapokuwa nyumbani kucheza dhidi ya Afc Bournemouth.
Mwamuzi huyo ndiye aliyesababisha Chelsea ikaadhibiwa msimu uliopita kutokana na wachezaji kumzonga kumlalamikia kutokana na kumaliza mpira wakati ambao Willian Borges alikuwa akijiandaa kupiga kona akapuliza filimbi kuashiria muda wa mapumziko wakati nyota huyo alikuwa bado hajapiga kona.

Mchezo uliopita:
Chelsea haikuwa na matokeo mazuri katika mchezo uliopita ambapo ilipoteza kwa magoli 0-3 dhidi ya Bournemouth. Mchezo ambao kocha Antonio Conte alikiri kwamba ulikuwa mchezo mbaya sana kwa Chelsea kwa jinsi ilivyozidiwa.

Uchambuzi:
Naona mchezo huu Chelsea ikija na mfumo wa kushambulia zaidi kutokana na kwanza ipo nyumbani lakini pia kutokana na kutaka kurejesha heshima iliyoipoteza msimu uliopita wakati ilipopoteza. Lakini pia huenda kocha Maurizio Sarri alitumia madhaifu ya mchezo uliopita dhidi ya Newcastle ambapo Chelsea ilipiga mashuti machache katika lango la timu pinzani licha ya kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa.

Muda: Saa 5:00 Jioni (Saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki.


û

No comments:

Post a Comment