Nyota na winga wa Chelsea ambaye amekuwa akiichezea sana klabu ya vijana ya Chelsea, Charly Musonda Jr amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Vitesse ya nchini Uholanzi.
Musonda Jr ambaye aliiongoza Chelsea ya vijana katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa vijana na kupewa kadi nyekundu uku Chelsea ikipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya vijana wa Leicester city amekamilisha uhamisho huo wa kujiunga na klabu hiyo ambayo imekuwa na mahusiano mazuri sana na klabu ya Chelsea ambapo wachezaji wengi waliowai kucheza kwa mkopo klabuni Chelsea wamekuwa wakipelekwa uko.
Klabu hiyo ya Vitesse imefanikiwa kuwanasa nyota kama Eduardo Carvalho ambaye ni mlinda mlango namba tatu wa Chelsea pamoja na Jake Clarke-Salter ambaye msimu uliopita alijiunga kwa mkopo na klabu ya Sunderland.
Wakati huohuo, nyota wa Chelsea ambaye ni raia wa Jamaica, Michael Hector amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Sheffield Wednesday ya nchini Uingereza.
Nyota huyo tangu amejiunga na Chelsea hajafanikiwa kuichezea mchezo wowote wa kimashindano uku akisajiliwa na Chelsea kutoka klabu ya Reading.
Jambo ambalo labda utashangaa kuhusu nyota huyu ni kwamba wakati kwasasa akiwa na miaka 26 tayari ameshasajiliwa kwenye klabu 16 uku klabu mbili tu ndizo alizozitumikia kama mchezaji rasmi. Ni Chelsea na Reading tu lakini klabu nyengine zote amekuwa akichezea kwa mkopo.
Lakini pia nyota mwengine mwenye miaka 21 kwasasa nyota na mlinda mlango wa Chelsea, Bradley Collins amekamilisha mkopo wake wa pili wa kujunga na klabu ya Burton Albion.
Bradley ambaye kwa ufupi anaitwa Brad amekamilisha mkopo wake huo wa pili wa kujunga na klabu hiyo ya nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment