Kocha Sarri atoa ufafanuzi kuhusu Willian na Pedro - Darajani 1905

Kocha Sarri atoa ufafanuzi kuhusu Willian na Pedro

Share This

Mchezo uliopita kati ya Chelsea dhidi ya Afc Bournemouth, Chelsea ilianzisha kikosi ambacho kilibadilika katika nafasi moja tofauti na kikosi kilichopita wakati Chelsea ilipoondoka na ushindi wa mabao 1-2 dhidi ya Newcastle. Ilibadilika katika nafasi ya Pedro Rodriguez ambaye kwenye mchezo dhidi ya Newcastle alianza, lakini kwenye mchezo huu dhidi ya Afc Bournemouth alisubiri benchi.

Mara baada ya mabadiliko hayo, kocha Maurizio Sarri aliulizwa kwanini aliamua kumwanzisha Willian uku Pedro akisubiri, kocha Sarri alijibu na kusema kwamba "Katika michezo mitatu yote iliyopita (ya ligi kuu Uingereza), tulianza na Pedro, lakini katika mchezo huu (dhidi ya Bournemouth) niliona itakuwa vyema zaidi nikaanza na Willian."

"Najiona kocha mwenye bahati sana. Kwa nafasi moja kuwa na mtu kama Willian na Pedro ni jambo zuri na kubwa sana kwangu. Najiona nina bahati kuwa na watu kama Willian, Pedro na Moses ambao wote kwa pamoja wanacheza vizuri" alisema Sarri..

Chelsea imekuwa ikicheza kwa mfumo wa 4-3-3 uku ikiwatumia washambuliaji watatu ambao ni pamoja na Eden Hazard, Alvaro Morata uku katika nafasi ya winga wa kulia ikiwa na watu kama Willian, Pedro na Victor Moses.

No comments:

Post a Comment