Mchezaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard amenukuliwa akidai kupendezwa zaidi na mbinu za kocha wa sasa klabuni hapo Maurizio Sarri ukilinganisha na mbinu za makocha wawili waliopita yaani Jose Mourinho na Antonio Conte.
Sarri anatajwa kufanikiwa kwa asilimia 100 baada ya kushinda mechi zote nne za mwanzo na kujikusanyia alama 12 sawa na Liverpool na Watford ila tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ikiwaweka Liverpool kileleni mwa ligi.
Akimzungumzia kocha huo muitaliano, Hazard amesema "kocha hapendi kabisa mpira ukae nyuma yaani golini kwetu, anapenda tuucheze angalau mita 30 kutoka kwenye goli la wapinzani na kama mpira utakua golini kwetu basi tunajukumu la kuuondoa kwa haraka sana"
"tunalifanyia sana mazoezi hili jambo na ni mbinu endelevu"
"huwa napenda sana kumiliki mpira na kwa mbinu hii nafikiri ni moja kati ya vitu vinavonipa hamasa ya kukaa na mpira hasa upande wa wapinzani"
"nimeipenda sana hii mbinu ya kucheza kwa haraka hasa katika lango la wapinzani ni mbinu nzuri zaidi ukilinganisha na mbinu za makocha waliopita"
Lakini pamoja na yote Sarri bado hajalizishwa na kasi ya timu yake kwa sasa na anadai bado wanakazi ya ziada ya kufanya.
No comments:
Post a Comment