Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea pamoja na timu ya taifa ya Uingereza, John Terry huenda akarejea uwanjani akiwa kama mchezaji kwa mara nyengine tena mara baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na klabu aliyoitumikia msimu uliopita, Aston Villa.
Ripoti iliyoripotiwa na magazeti ya nchini Uingereza yanadai gwiji huyo aliyedumu klabuni Chelsea kwa miaka 22 uku akiwa nahodha kwa miaka 13 ameshawishia na kocha Steve Bruce ili arejee tena klabuni Aston Villa ili aitumikie kwa msimu mwengine.
Steve Bruce ambaye ni kocha wa klabu hiyo ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championships inadaiwa amewaeleza wamiliki wapya wa klabu hiyo kwamba anahitaji John Terry apewe mkataba mwengine wa mwaka mmoja ili aitumikie klabu hiyo inayopambana kurejea ligi kuu.
Msimu uliopita, John Terry alikuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa kilichopambana kushiriki ligi kuu Uingereza lakini waliishia kupoteza mbele ya Fulham kwa goli 1-0 katika mchezo wa fainali ya mtoano na kushindwa kufudhu kurejea ligi kuu.
Kocha huyo raia wa Uingereza anakiri kwamba John Terry alishiriki kwa kiasi kikubwa kuiwezesha klabu hiyo kucheza mchezo huo wa fainali ya mroano (play-off) hivyo kutamani kuungana tena na mlinzi huyo ambaye kwasasa hana timu anayoichezea.
Wakati huohuo, John Terry amechaguliwa kushiriki mchezo wa hisani kwa ajili ya uchangiaji wa pesa ili kutoa msaada kwa wagonjwa wa ugonjwa wa saratani.
Kupiria mtandao wa Instagram, John Terry alituma ujumbe akisema atakuwa moja ya washiriki katika mchezo huo ulioandaliwa na nyota wa klabu ya Liverpool, James Milner pamoja na mwanasoka wa zamani wa klabu ya Celtic, Stiliyan Petrov ambao wao ndio watakaotengeneza timu mbili kucheza mchezo huo wa hisani..Mchezo huo utachezwa jumamosi hii ya tarehe 5-Septemba uko nchini Uingereza. John Terry atacheza upande wa timu ya Petrov.
No comments:
Post a Comment