Tarehe 31 ya mwezi uliopita ndio ilikuwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili barani Ulaya. Hivyo klabu zote barani humo haziruhusiwi kusajili mchezaji yoyote (tofauti na wale wachezaji ambao wapo huru yaani hawana mkataba na timu yoyote).
Kufungwa kwa dirisha hilo la kipindi cha kiangazi kulimaanisha pia kwamba kila klabu ilitakiwa kupeleka orodha kamili ya wachezaji itakakaowatumia kwa nusu msimu kabla ya kufunguliwa tena dirisha dogo la mwezi Januari lakini sheria hiyo inakuwa tofauti na timu zinazoshiriki michuano ya Ulaya kama michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) na ligi ya Ulaya (Europa League) ambako huko wanahitaji wachezaji wa klabu kwa msimu mzima.
Chelsea nayo ni moja ya klabu zinazopatikana barani Ulaya kwenye nchi ya Uingereza hivyo nayo ilitakiwa kuorodhesha majina ya wachezaji 25 ambao watashiriki michuano ya ligi kuu Uingereza.
Na hatimaye jana ililitimiza jambo hilo kwa kupeleka majina ya wachezaji 25 ambao itawatumia kwa nusu msimu kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili la mwezi Januari.
Wachezaji ambao wamejumuishwa ni pamoja na wale wachezaji wanne waliosajiliwa kwenye dirisha la usajili hili lililofungwa ambao ni pamoja na Kepa Arrizabalaga kutoka Athletic Bilbao, Robert Green aliyekuwa mchezaji huru, Mateo Kovacic aliyetoka Real Madrid kwa mkopo na Jorginho Frello kutoka Napoli.
Kikosi kamili
Makipa: Kepa Arrizabalaga, Willy Caballero na Robert Green
Walinzi: Cesar Azpilicueta, Antonio Rudiger, Davide Zappacosta, Andreas Christensen, Marcos Alonso, Emerson Palmieri, David Luiz, na Gary Cahill
Viungo: Victor Moses, Mateo Kovacic, Jorginho Frello, Ross Barkley, N'Golo Kante, Ruben Loftus-Cheek, Lucas Piazon, Danny Drinkwater na Cesc Fabregas
Washambuliaji: Eden Hazard, Alvaro Morata, Willian Borges, Pedro Rodriguez na Olivier Giroud

Lakini huenda unajiuliza wapo wapi wale makinda akina Ethan Ampadu na Callum Hudson-Odoi!
Ipo hivi kama mchezaji haujatimiza miaka 21 basi hajumuishwi kwenye kikosi hiki cha wachezaji 25 lakini kama kocha akimuhitaji basi ataruhusiwa kumuita akitokea kikosi cha vijana. Nyota hao wote wana miaka 17 na wanacheza katika kikosi cha vijana cha Chelsea.
No comments:
Post a Comment