Nyota na mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Olivier Giroud amefanyiwa mahojiano na moja ya chombo cha habari kutoka nchini kwao Ufaransa na moja kati ya mambo aliyoulizwa na chombo hicho ni juu ya mustakabali wake klabuni Chelsea.
Nyota huyo ambaye aliiongoza timu yake ya taifa ya Ufaransa kushinda taji lake la Kombe la Dunia mwaka huu 2018 alipoulizwa swali hilo alisema bado ana furaha ya kusalia klabuni Chelsea lakini kubwa bado amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na klabu hiyo uku kukiwa na kipengele cha kusaini mkataba mpya hivyo anasubiri kama atasaini au atajiunga na klabu nyengine.
"Bado nna mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea, hivyo nadhani naweza kuendelea kubaki. Bado mazungumzo ya mkataba mpya hayajaanza, lakini kuna kipengele cha kusaini mkataba mpya. Kama itashindikana kusaini, basi nitaangalia sehemu nyengine nayoweza kutimkia" alisema nyota huyo mwenye miaka 31.
Giroud alijiunga na Chelsea katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari mwaka huu ambapo alisajiliwa kwa dau la paundi milioni 18 na kupewa mkataba wa miezi 18 hivyo kumaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment