Nyota wawili wa kikosi cha Chelsea wamekamilisha uhamisho wao wa kujiunga kwa mkopo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya hapo jana.
Ni Kylian Hazard pamoja na Tammy Abraham ambao wamejiunga kwa mkopo na klabu za Cercle Brugge na Aston Villa.
Kylian Hazard ambaye ni mdogo wa Eden Hazard amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Cercle Brugge inayopatikana nchini kwao Ubelgiji.
Nyota huyo amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kutaka kuondoka Chelsea kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha wakubwa uku akitumika tu kwenye kikosi cha vijana wa akademi ya Chelsea. Baba wa mchezaji huyo, Kylian Hazard aliwai kuripotiwa akisema mwanae huyo aliwai kufanyiwa majaribio na klabu ya VVV Venlo ya nchini Uholanzi lakini usajili wake ukashindikana.
Nyota huyo amejiunga kwa mkopo wa msimu mmoja ambapo mkataba wake wa mkopo unamalizika mwezi Juni mwakani. Alijiunga na Chelsea mwaka 2017 akitokea klabu ya Ujpest.
Wakati huohuo, nyota raia wa Uingereza, Tammy Abraham ambaye ni nyota zao la akademi ya Chelsea emekamilisha uhamisho wake wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Aston Villa ambayo nayo inapatikana ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championships.
Abraham amejiunga kwa mkopo na klabu hiyo ikiwa msimu uliopita alitumika pia kwa mkopo kwenye klabu ya Swansea kabla ya kurejea klabuni Chelsea mara baada ya kumalizika kwa msimu.
No comments:
Post a Comment