Makundi ya Europa yapangwa, Chelsea yapewa vibonde - Darajani 1905

Makundi ya Europa yapangwa, Chelsea yapewa vibonde

Share This

Chelsea ni kama inaanza rasmi mbio zake katika michuano ya msimu huu wa 2018-2019 mara baada ya hapo jana kupangwa kwa makundi ya Europa League na klabu ya Chelsea kuwemo kwenye moja ya makundi hayo ambapo inaonekana kuwa rahisi sana kwa Chelsea kuweza kufanikiwa kufudhu katika hatua hiyo ya makundi.

Chelsea imepangwa katika kundi moja na klabu ya PAOK kutoka nchini Ugiriki, Bate Borisov kutoka nchini Belarus na klabu ya Vidi FC kutoka nchini Hungary.

Klabu hizo zote zimepangwa katika kundi L uku kukionekana kwa asilimia kubwa Chelsea kukosa mpinzani katika kundi hilo ambapo ana nafasi kubwa ukizangatia na historia yake ya kuwai kushinda taji hilo mwaka 2013 ilipokuwa chini ya kocha Rafa Benitez.

No comments:

Post a Comment