Terry akataa kuondoka Uingereza, apokea ofa kutoka Chelsea - Darajani 1905

Terry akataa kuondoka Uingereza, apokea ofa kutoka Chelsea

Share This

Gwiji wa Chelsea, John Terry amekuwa akihusishwa kutakiwa na klabu kadhaa ambazo ni pamoja na Spartak Moscow kutoka nchini Urusi, Sporting Lisbon kutoka nchini Ureno na klabu ya Aston Villa ambayo amemaliza nayo mkataba mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kuichezea kwa msimu mmoja.

Taarifa za mwisho zilikuwa kwamba nyota huyo ameshafanyiwa vipimo na klabu ya Spartak Moscow kutoka nchini Urusi na ilikuwa imebakiza hatua za mwisho ili usajili huo ukamilike uku ikielezwa klabu hiyo ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 1.8 kama mshahara wake wa mwaka mara baada ya kukatwa kodi.

Lakini sasa usajili huo ni kama umeshavunjika.
Hiyo ni mara baada ya gwiji huyo raia wa Uingereza kutuma ujumbe kupitia mtandao wa Instagram ambapo ametuma ujumbe akisema ameachana na mpango wa kujiunga na klabu hiyo uku sababu akisema ni mara baada ya maamuzi ya familia yake ambapo amekaa nayo na kujadiliana na kuona usajili huo wa kusafiri mpaka nchini Urusi hautokuwa mzuri kwao.

Kumbuka katika maisha yake ya soka, mlinzi huyo hajawai kutoka na kwenda kucheza soka nje ya Uingereza akiwa kama mchezaji wa klabu flani.hivyo kuwa ugumu kwa familia yake ambayo imeshatengeneza kujiwekeza nchini kwao Uingereza.

Watoto wake wawili mapacha na mke wake Toni Terry inadaiwa wamekataa usajili huo hivyo inamlazimu Terry mwenye miaka 37 kusalia nchini Uingereza ingawa hana timu.
Chelsea ni moja ya klabu inayotajwa kumpa ofa ya mkataba wa kurejea Chelsea akiwa mmoja wapo wa makocha au watu wa benchi la ufundi.

No comments:

Post a Comment