Atalanta wanataka kumnasa jumla nyota wa Chelsea - Darajani 1905

Atalanta wanataka kumnasa jumla nyota wa Chelsea

Share This
Klabu ya Atalanta inayoshiriki ligi kuu nchini Italia inataka kuingia sokoni kujaribu kumsajili nyota wa Chelsea aliyepo kwa mkopo klabuni humo, Mario Pasalic.

Nyota huyo raia wa Croatia alijiunga kwa mkopo na klabu hiyo mwaka 2018 na amekuwa na msimu mzuri mpaka sasa akicheza michezo 22 ya ligi kuu kwa msimu huu na kuhusika kwenye magoli 8 akifunga matano na kutoa pasi ya mwisho magoli matatu.

Inaelezwa Atalanta imetenga euro milioni 15 ili kumnasa nyota huyo mwenye miaka 25.

No comments:

Post a Comment