Chelsea kuivaa Man utd hii leo kwenye mbio za kuwania Ubingwa - Darajani 1905

Chelsea kuivaa Man utd hii leo kwenye mbio za kuwania Ubingwa

Share This
Chelsea Women leo inashuka uwanjani kwa mara nyengine tena kucheza mchezo wake wa 14 wa ligi kuu ya soka la wanawake nchini Uingereza ambapo leo kwa mara nyengine tena itakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Man utd Women.


Chelsea Women inashuka uwanjani hii leo mara baada ya mchezo uliopita kupata ushindi mnono wa mabao 8-0 dhidi ya wanawake wa West Ham, mchezo uliochezwa jumapili ya tarehe 2-Februari.

Lakini pia kabla ya mchezo huo Chelsea ilimenyana dhidi ya wanawake hawahawa wa Man utd kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Ligi maarufu kama Continental Cup na Chelsea ikatinga hatua ya fainali kwa ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na nyota mkongwe, Maren Mjelde.


Mchezo wa leo ni mchezo muhimu kwa Chelsea katika mbio zake za kuwania ubingwa wa ligi kuu ambapo kwasasa inashika nafasi ya pili uku ikiwa imecheza michezo pungufu ikizidiwa mchezo mmoja na ratiba inavyotakiwa kuwa ikiwa ina alama 35 uku Man city Women walio kileleni wakiongoza wakiwa wana alama 36.

Man utd Women wenyewe wamezidiwa alama 16 na Chelsea Women uku wakishika nafasi ya nne wakiwa wana alama 19.

No comments:

Post a Comment