ANTONIO CONTE KUELEKEA MCHEZO WA CARABAO - Darajani 1905

ANTONIO CONTE KUELEKEA MCHEZO WA CARABAO

Share This

Mchana wa leo kocha wa Chelsea, Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wa kesho wa kombe la Carabao ambapo Chelsea itamenyana na AFC Bournemouth katika hatua ya Robo fainali ya kombe ilo

Makinda kupewa nafasi
Katika mchezo huo inatarajiwa makinda kupata nafasi kwa kiasi kikubwa, ambapo Conte amesema watakaocheza mchezo huo ni wale wanaostahili akiwataja makinda kama Callum Odoi na Dijon Sterrling ambao wametokea kwenye akademi ya Chelsea akiwataja kama wanaweza kupata nafasi huku akisema Nathan Ampadu anaweza akaanza.

Batshuayi nae ndani
Mara baada ya kutoka majeruhi Michy Batshuayi anaweza akaanza na sio kusubiri mtu atoke ambapo toka atoke majeruhi amecheza mchezo mmoja tu huku akiingia kama mchezaji wa akiba.

Musonda na Luiz bado kuwa nje
Lakini pia alieleza Charly Musonda kuendelea kusumbuliwa na majeruhi huku David Luiz akiendelea kukosekana kutokana na majeruhi.

No comments:

Post a Comment