Kuelekea katika michuano yenye mvuto zaidi katika bara la Ulaya na duniani pia, Ligi ya Mabingwa Ulaya, ni mchezo mmoja tu unaotazamwa kuleta radha halisi ya maana ya ligi ya mabingwa ambao utawakutanisha mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza dhidi ya bingwa mtetezi wa Copa del Ley ambalo kombe la mfalme nchini Hispania, Barcelona.
Mchezo huo wa hatua ya 16 bora utaanzia katika uwanja wa Chelsea wa Stamford Bridge kabla ya kumalizia Camp Nou ambao ni uwanja wa Barcelona.
Kuelekea katika mchezo huo, kumekuwa na kauli na tabiri nyingi zikitolewa lakini kwa mchambuzi wa soka, Michael Deberry ambaye aliwai kuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, mwenyewe anaamini yoyote anaweza kushinda mchezo huo ambapo ni sawa na wacheza masumbwi, yoyote anaweza kumpiga ngumi mwenzake na kushinda mchezo.
Lakini mchambuzi huyo anaamini pia kuwa Chelsea ina nafasi kubwa ya kufuzu na inaweza kumzuia mshindi wa tunzo ya dunia ya mchezaji bora mara 5, Lionel Messi.
Deberry anaamini katika michezo nane ambayo Messi amekutana na Chelsea hajawai kuifunga na anaamini katika hilo huenda likatokea tena.
No comments:
Post a Comment