"DIEGO COSTA NA DAVID LUIZ HAIJAELEWEKA BADO" - Darajani 1905

"DIEGO COSTA NA DAVID LUIZ HAIJAELEWEKA BADO"

Share This
Ikiwa kumetimia nusu ya msimu wa ligi kuu Uingereza, jarida au gazeti la moja linaloitwa Guardian ambalo huwa linaandika habari za michezo limefanya tathmini kwa mashabiki wa klabu za Uingereza kuhusu jinsi wanavyoziona timu zao ambapo kwa upande wa shabiki wa Chelsea, Trizia Fiorelli

Msimu huu anauonaje?
" Kiukweli ni msimu mzuri, sio mbaya na hatulalamiki maana kila mtu anajua ukubwa wa Manchester city msimu huu, na hatupingi kuwa nafasi ya tatu kwenye ligi lakini inatuuma kupoteza alama muhimu katik michezo ya Crystal Palace na West Ham. Kwa hapo timu naipa alama 7/10 ya kufanya vizuri''

Waliong'aa na walioboronga
"Hazard na Kante bado wanaendelea kuwa nyota wa muhimu kwetu, na huwa tunapata tabu pale ambapo mmoja akikosekana, Alvaro Morata nae amekuwa akifunga magoli ya muhimu ambapo hiyo ndio sababu tuliyomnunulia"
"kwa walioboronga, Victor Moses hayupo sawa, japo kwa wengi hawaliongelei hilo, amekuwa hayupo sawa, mdhaifu sana, hayupo sawa kiujumla"

Je mnamfurahia kocha(Antonio Conte)?
"Ni ngumu kuelewa haswa kilichotokea kwa Diego Costa, na kuporomoka kwa David Luiz na klabu kushindwa kuendana na matamanio ya kocha katika kufanya usajili ambayo hiyo ni kama imehathiri. Mashabiki wengi wa Chelsea bado wana furaha na kocha, ambapo wanaamini hivi karibuni mambo yatakuwa sawa. Kwa hapo Conte anapewa 8/10."

Kipindi gani kimekuwa bora zaidi kwa Chelsea kwa mwaka 2017?
"Kuishuhudia Chelsea ikipambania kombe la ligi kuu ikishindana na Tottenham"
Hayo ni maoni yake kama shabiki wa Chelsea, je wewe kama shabiki wa Chelsea au mtu wa soka, unapingana nae wapi?

No comments:

Post a Comment