HABARI MBAYA ZINAZOMHUSU KANTE - Darajani 1905

HABARI MBAYA ZINAZOMHUSU KANTE

Share This
Hii ni zaidi ya habari mbaya kwa mashabiki wa Chelsea duniani kote. Ni habari ambayo hakuna shabiki na mpenzi wa Chelsea hatopenda zitokee na hata ziwe na chembe ya ukweli ndani yake, habari zilizozagaa kwenye vyombo vingi vya habari ni kuwa iungo wa Chelsea, N'Golo Kante anatakiwa na wababe wa Ulaya ambao ni Real Madrid na PSG.

Kuna taarifa kuwa klabu hizo zimetupa nyavu zao kwa nyota huyo wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa ambaye jana alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ufaransa kwa mwaka 2017 anatakiwa na klabu hizo.

Akihojiwa kuhusu tetesi hizo, Kante alisema "Nina taarifa za kutakiwa na Olympique Marseille tu, ila nitafanya maamuzi nijue nini cha kufanya"

Hii ni habari mbaya zaidi kuwai kuzipata katika kipindi hichi ambacho timu ipo chini ya kocha Antonio Conte, nadhani katika hili bodi ya Chelsea inabidi ifanye haraka iwezekanavyo ikiwezekana imuongezee hata mshahara maana sio jambo zuri kumpoteza mt kama Kante, ambaye ana msaada mkubwa katika timu.

1 comment: