KOCHA CONTE AONGELEA USHINDI vs BRIGHTON - Darajani 1905

KOCHA CONTE AONGELEA USHINDI vs BRIGHTON

Share This

Ni siku nyengine tamu kwa mashabiki wa Chelsea, kote duniani mara baada ya klabu yetu pendwa kupata ushindi muhimu dhidi ya Brighton katika mchezo wa 20 wa ligi kuu Uingereza.

Katika mchezo huo ambao Chelsea imeshinda 2-0 huku magoli yakifungwa na Alvaro Morata akipokea pasi kutoka kwa Cesar Azpilicueta na jengine likifungwa na Marcos Alonso akifunga kwa kwa kichwa baada ya kupigwa kona na kiungo Cesc Fabregas.

Mara baada ya mchezo kocha Antonio Conte aliongelea mchezo huo akiwa na waandishi wa habari, n hichi ndicho alichokisema;

Kuhusu ushindi dhidi ya Brighton;
Conte alijibu "ni jambo zuri, maana mchezo wote tuliutawala sisi, tumepiga mashuti 25 huku nane yakienda golini, haikutakiwa twende mapumziko tukiwa hatujapata goli maana tulistahili kama tulivyostahili kwa Everton ingawa hii ya leo wachezaji wamefanya kazi kubwa kuleta matokeo mazuri, nawapongeza kwa hilo"

Anamuongeleaje mlinzi Marcos Alonso?
Conte alijibu "ni mchezaji mzuri, na mpaka sasa ashafunga magoli matano ambayo kwake ni hatua na mafanikio makubwa sana, ila asiache kufunga maana magoli yake yanatupatia ushindi (anacheka)"

Vipi kuhusu Azpilicueta na Morata, anawaongeleaje?
Conte alijibu "Azpilicueta anatimiza pasi ya mwisho 'assist' ya sita, ila nae inabidi afunge sio kutoa pasi kila siku (anatania na kucheka). Amekuwa akitoa pasi nzuri na miguu yake ina nguvu kubwa, ila kwa Morata inabidi afanye mpango amtoe akamnunulie zawadi ambapo katika kutoka huko nae anaweza kualikwa akaenda (anacheka tena)"

Anaongeleaje nafasi yake katika kulitetea taji la ligi kuu?
Conte alijibu "bado ni ngumu kusema unapambana kushindana na Mama site (Manchester city iliyo kileleni) maana kila siku wanafanya maajabu na kuzidi kujiweka kileleni vizuri"

Je vipi Morata alishazoea kucheza kipindi cha 'Christmass', hapati tabu?
Conte alijibu "tena sio Morata tu, kuna Bakayoko na Antoinne Rudiger wote hawakuzoea kucheza kipindi kama hichi lakini hakuna tabu kucheza kipindi kama hichi maana hali inakuwa shwari, lakini pia kutokana na sikukuu ya 'Christmass' inawapa fursa ndugu na majamaa zao ambao wametoka katika nchi nyingi kuweza kufika uwanjani kuweza kumuona ndugu yao"

Na vipi kuhusu tetesi za Artulo Vidal?
Conte alijibu "huwa sipendelei kuongelea wachezaji wa timu pinzani, ila kwa Alvaro (mwandishi anamkosoa na kumrekebisha-Ni Arturo)" Conte ananyamaza kidogo huku akicheka na anaendelea "si unaona navyowapenda wachezaji wangu, sawa Artulo Vidal nampenda sana ambapo tulishawai kufanya kazi pamoja Juventus, namkubali na natamani niungane nae tena"

*Naona leo kocha Antonio Conte anacheka tu,  hii ndio furaha ya Chelsea ambayo mashabiki tunapenda tuione ikiwa hivi kila siku.

No comments:

Post a Comment