MJUKUU WA MENDOZA ANAZIDI KUUWASHA MOTO - Darajani 1905

MJUKUU WA MENDOZA ANAZIDI KUUWASHA MOTO

Share This
Unaambiwa ni hatari! Anaitwa Marcos Alonso Mendoza, ndilo jina kamili alilopewa baada ya kuja duniani miaka 26 iliyopita, kama haujui tu kesho anafurahia kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, anatimimiza miaka 27 rasmi, lakini anakaribia kutimiza miaka hiyo akiwa na rekodi nzuri kwenye ligi kuu Uingereza.

Unaambiwa Mendoza huyu ndiye beki au mlinzi anayeongoza kufunga magoli toka awasili katika ligi hiyo akiwa na uzi wa Chelsea. Akifunga magoli 11 mpaka sasa.

Lakini kama haukuwai kujua, jamaa huyu aliwai kuzichezea klabu za Bolton Wanderers iliyowai kushiriki ligi kuu uingereza, na kama una kumbukumbu vizuri, Gary Cahill ambaye ndiye nahodha wa Chelsea alisajiliwa akitokea klabu hiyo na pia Mendoza aliwai kuichezea Sunderland kwa mkopo.

Huyu ndiye Mendoza ambaye jana alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo ambapo Chelsea ilipomenyana na Brighton huku Chelsea ikishinda 2-0 na Mjukuu huyo wa Mendoza kufunga kwa kichwa.

Sasa kwa moto huu wa mjukuu wa Mendoza, kuna haja gani ya kumleta huyo Alex Sandro? Hahaaaaa natania jamani, ili timu iwe na kikosi cha ushindani, inatakiwa iwe na kikosi kipana.

Hongera MArcos Alonso Mendoza a.k.a Mjukuu wa Mendoza

1 comment:

  1. kati ya LeftBack nazo zikubari dunian kwasasa ni pamoja na Marcos Alonso Mendoza, ni aina ya Fullback ambazo zinakabwa ( hazikabi ) ukimlinganisha na Marcelo wa Madrid

    ReplyDelete