Mara baada ya Chelsea kufanikiwa kuvuka katika hatua ya robo fainali ikiifunga Afc Bournemouth kwa magoli 2-1 katika kombe la ligi la Carabao Cup na kisha kupangiwa kucheza na Arsenal katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo, ambapo mchezo huo utachezwa mwezi januari, kuna taarifa mpya imetoka kuhusu nusu fainali ya kombe hilo.
EFL ambao ndio wanasimamia kombe hilo wametangaza kutumika kwa teknolojia ya Video Assistant Referee(VAR) ambayo yenyewe inatumika pale ambapo mwamuzi wa mchezo anakuwa hana uhakika na tukio lililotokea uwanjani.
Lakini teknolojia hiyo imekuwa ikilalamikiwa sana kutokana na kupoteza radha ya mchezo wa soka ambapo mwamuzi anategemea maamuzi kwa marefa wa pembeni wanaoangalia mchezo huo kupitia televisheni.
Chelsea ndiyo itakuwa mara ya kwanza kutumia mfumo huu ambapo hapo kabla haijawai kuitumia.
Arsenal wataanza kusafiri kuifata Chelsea katika michezo hiyo ya nusu fainali katika uwanja wa Stamford Bridge na kama mchezo utaisha suluhu ndipo Arsenal watapata fursa ya kucheza nyumbani kwao Fly Emirates Stadium
*mfumo huo utatumika pia katika mchezo wa fainali
No comments:
Post a Comment