Mshambuliaji wa Chelsea ambaye anaichezea Swansea kwa mkopo akiwa ametokea kwenye akademi ya Chelsea, Tammy Abraham amefanya mahojiano mafupi huku akiielezea Chelsea.
Kuhusu ukame wake wa kufunga
Tammy alijibu "ni kipindi kigumu kwangu, ila sioni tatizo sana maana najua kila mshambuliaji wa soka aliwai kupitia kipindi kama hiki"
Kuhusu ubovu wa klabu anayochezea kwa sasa(Swansea) inayoshika mkia ligi kuu
Tammy alijibu "ni jambo gumu kwangu kama mchezaji maana napenda kuona timu inafanikiwa, lakini ni nzuri pia kwangu maana najifunza kupitia kipindi kigumu kama hiki ukizingatia nilipokuwa kwenye akademi ya Chelsea tulikuwa tumezoea kushinda"
Kocha Antonio Conte huwa anaongeaga nae
Tammy alijibu "huwa nafanyaga mawasiliano nae sana, na naongea nae sana ingawa kuna kipindi huwa simuelewi (Anacheka-Conte ni muitaliano kwa hiyo kiingereza chake hakipo vizuri) lakini huwa namuelewa na mara zote huwa ananihusia nipambane zaidi.
Huwa unajiskiaje unapocheza na wale uliokuwa nao
Tammy alijibu "huwa ni jambo zuri kwangu kucheza na yule mtu uliyekuwa nae pamoja mkiwa kwenye akademi"
Baadhi ya wachezaji walioko kwa mkopo katika timu za Uingereza kutoka Chelsea; Tammy Abraham (Swansea), Ruben Loftus-Cheek (Crystal Palace), Jeremie Boga (Birmgham City), Kurt Zouma (Stoke city)
No comments:
Post a Comment