CARABAO; FT, CHELSEA 0-0 ARSENAL - Darajani 1905

CARABAO; FT, CHELSEA 0-0 ARSENAL

Share This

Ni sare nyengine inapatikana katika michezo minne ya mwisho kukutana kwa timu hizo, Chelsea ilitengeneza nafasi nyingi ambazo kama ingekuwa makini basi ingepata matokeo mazuri.

Nafasi kadhaa Chelsea imetengeneza bila kufanikiwa kupata magoli mashuti zaidi ya 20 yalipigwa golini kwa Arsenyani(Arsenal) ila mwisho wa siku hakuna aliyeibuka mbabe.

Ila hongera kwa safu ya ulinzi iliyoongoza na nahodha msaidizi Cesar Azpilicueta huku akiwa na Andreas Christensen na Antonio Rudiger, wameonyesha ukomavu mkubwa na kucheza soka safi.

N'Golo Kante alifanya kama kawaida yake kukata umeme na kuwahakikishia usalama mabeki na kipa wao, huku pia Cesc Fabregas na Danny Drinkwater wakijaribu kuionganisha vyema safu ya ushambuliaji kwa kutengeneza nafasi kadhaa.

Ila naona kuna umuhimu mkubwa wa Victor Moses kuweza kufanya kazi kubwa kurudi katika kiwango chake maana anaonekana kufanya baadhi ya makosa ambayo huenda yakamgharimu kupoteza nafasi yake kwa muitaliano Davide Zappacosta.

Alvaro Morata, leo amejaribu kuonyesha umakini golini, amejitahidi kwa uwezo wake ila hakuwa na nafasi ya kufunga tu. Marcos Alonso, Eden Hazard na Willian aliyeingia kama mchezaji wa akiba hawakuwa na tatizo sana.

Sasa kazi ni kuangalia mchezo ambao Chelsea itakuwa ugenini siku ya tarehe 24-Januari ambapo mshindi wa hapo maana yake atafanikiwa kucheza fainali ya michuano hiyo ya Carabao.

No comments:

Post a Comment