CHELSEA KUACHANA NA MDOGO WA HAZARD - Darajani 1905

CHELSEA KUACHANA NA MDOGO WA HAZARD

Share This

Kuna taarifa zinadai kuwa Chelsea ipo tayari kuachana na nyota wa klabu hiyo, Kylian Hazard ambaye ni mdogo wa nyota wa sasa wa Chelsea, Eden Hazard na huenda ikamtoa kwa mkopo au kumuuza katika dirisha kubwa la usajili la kipindi cha kiangazi.

Chelsea ilimvuta kinda huyo aliyedumu klabuni Chelsea akiwa kwenye akademi ya Chelsea huku akiwa na miezi isiyozidi mitano toka asajiliwe anataka kuondoka klabuni hapa ili akatafute timu atakayoweza kupata nafasi ya kucheza ambapo kwa sasa ana miaka 22.

Baba wa nyota huyo, Thierry Hazard aliwai kukaririwa akisema anamtafutia mwanae klabu nyengine ili akapate nafasi akitaka kumtoa klabuni Chelsea ambapo kaka yake yupo hapo toka mwaka 2013.

Hii sio mara ya kwanza kwa mdogo wa Eden Hazard kutua klabuni hapo na kuungana na kaka yake, alianza nyota wa sasa wa klabu ya Borrusia Monchnglebach ya nchini Ujerumani, Thorgan Hazard ambaye naye alisajiliwa na Chelsea na akaishia kutolewa kwa mkopo na mwisho kuuzwa kabisa. Na sasa inatokea tena kwa huyu ambaye yeye haijajulikana kama atauzwa kabisa au atatolewa kwa mkopo ifikapo mwezi Juni.

No comments:

Post a Comment