Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameelezea tatizo linaloikumba Chelsea kwa sasa mpaka kuifanya inashindwa kufunga magoli, ambapo katika michezo mitatu ya mwisho iliyocheza klabu hiyo imeshindwa kufunga goli lolote.
"Nadhani tatizo lipo kwa timu nzima, sio kwa Morata na hata kwa Batshuayi ata akipata nafasi ya kucheza. Tunatengeneza nafasi nyingi, lakini tunashindwa kuzitumia na kufanya ziwe magoli. Ni tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, tulikuwa tunaruhusu magoli machache lakini ushindi ulikuwepo" alisema kocha huyo ambaye anaiongoza Chelsea kwa msimu wake wa pili sasa huku akiisaidia kushinda taji moja la ligi kuu Uingereza msimu uliopita.
"Inatakiwa tupambane kuhakikisha tunalimaliza tatizo hili" alisema kocha huyo
Na alipoulizwa juu ya mfumo wa Chelsea wa sasa wa 3-5-2 huku wengi wakimshauri atumie mfumo wa 3-4-3 ambao ndio ulioisaidia Chelsea kutwaa taji hilo msimu uliopita alisema "Tatizo sio mfumo, maana hata kwenye mechi dhidi ya Norwich tulitumia 3-4-3 na bado tulishindwa kufunga. Tatizo lililopo ni mfumo wa timu, inabidi tupambane katika hilo la kubadili mfumo" alisema kocha Antonio Conte.
No comments:
Post a Comment