Klabu ya Paris St.Germain au maarufu kama PSG ya nchini Ufaransa inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama Ligue 1 inamsaka nyota wa nchini humo, N'Golo Kante ambaye amekuwa tegemeo kwenye nafasi ya kiungo ya Chelsea huku akiisaidia kuwa bingwa wa Uingereza msimu uliopita na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu kwa msimu huo.
Klabu ya PSG, iliyochini ya kocha Unai Emery inamtaka nyota huyo aungane na klabu hiyo na inatajwa kumfanya kuwa chaguo la kwanza.
N'Golo Kante ambaye pia aliwai kuhusishwa kutakiwa na klabu kama Real Madrid na Olympique Marseille aliwai kuhojiwa juu ya kutakiwa na klabu kadhaa naye alijibu "Nilisikia kuna ofa moja ya kutoka Marseille, lakini nitafikiria na kufanya uamuzi"
No comments:
Post a Comment