Nyota wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard ambaye aliichezea Chelsea kwa mafanikio makubwa akifanikiwa kushinda mataji matatu ya ligi kuu Uingereza na ligi ya mabingwa Ulaya mara moja amemjia juu kiungo wa sasa wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko juu ya kiwango alichokionyesha kwenye mchezo wa jana ambapo Chelsea ilitoka sare ya 0-0 dhidi ya Leicester.
"Anaonekana hayupo sawa, hana kasi na bado anaonekana kutokucheza kwa kujiamini. Nadhani anatakiwa ajaribu kufanya juhudi ili awe sawa kwenye kiwango" alisema nyota huyo alipokuwa anauchambua mchezo huo ambapo kwa suluhu iliyopatikana imeifanya Chelsea itimize alama 49.
Lakini pia mchambuzi mwengine wa soka aliyekuwa pamoja na Frank Lampard, Ian Wright alimuongelea pia nyota huyo akisema "Ameanza michezo 17 kati ya 23 msimu, na huu ni mwezi Januari, nadhani ameshaizoea ligi na anatakiwa kupambana zaidi"
Je una maoni gani kuhusu kiwango cha Bakayoko?
No comments:
Post a Comment