CONTE AMTAKA SUAREZ WA BARCELONA - Darajani 1905

CONTE AMTAKA SUAREZ WA BARCELONA

Share This

Mara baada ya Chelsea kufululiza michezo mitatu bila kufunga, kocha wa Chelsea, Antonio Conte anatajwa kumfukuzia mshambuliaji wa klabu ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga, Denis Suarez ili aungane na Chelsea katika kusaidia safu ya ushambuliaji.

Chelsea imekuwa na mfululizo wa matokeo mabovu ikitoa suluhu katika michezo minne kwa mashindano yote huku ikishindwa kufunga goli katika michezo mitatu na sasa inataka kumvuta nyota huyo mwenye miaka 24 na siku 8 ambaye ametoka kutimiza umri huo siku ya tarehe 06-Januari anatazamiwa kujiunga na Chelsea ili kuwa changamoto kwa mshambuliaji wa sasa Alvaro Morata huku Michy Batshuayi akitajwa kujiunga kwa mkopo kwenye klabu ya Sevilla.

Denis Suarez amekuwa na ugumu wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza huku Luis Suarez na Lionel Messi wakionekana kumpa tabu nyota katika kupambania nafasi katika kikosi hicho na huenda akatafuta klabu nyengine ili aweze kupata nafasi.

No comments:

Post a Comment