SANDRO KARIBUNI KUUZWA, CONTE NA MOURINHO VITANI - Darajani 1905

SANDRO KARIBUNI KUUZWA, CONTE NA MOURINHO VITANI

Share This

Mara baada ya mfululizo wa kurushiana maneno baina ya makocha wawili, Antonio Conte wa Chelsea na Jose Mourinho wa Manyumbu(Man utd) ambaye alishawai kuifundisha Chelsea kabla ya Conte sasa ugomvi huo tena unatajwa kuhamia kwa nyota wa klabu ya Juventus ambaye ni raia wa Brazil, Alex Sandro.

Kila mmoja anamtaka nyota huyo ingawa haijajulikana nani atashinda vita hii, kwa vita ile ya maneno inaonekana ni kama imenyamaza flani kutokana na kauli ya Conte aliposema anataka apambane na Mourinho uso kwa uso tarehe 25-Februari ambapo Chelsea itasafiri mpaka Old Trafford kumenyana na Manyumbu.

Sasa vita hii nayo inatajwa kuwaweka makocha hao kwenye ushindani. Antonio Conte anamtaka mlinzi wa kushoto ambaye anataka kumpa changamoto mlinzi wa sasa wa Chelsea kwa nafasi hiyo Marcos Alonso wakati Mourinho alipohojiwa kuhusu uhitaji wa mlinzi huyo alisema "Naona Alex Sandro ndiye anaweza kulitatua tatizo la Man utd kwa upande wa mlinzi wa kushoto" sasa wote wawili wanaonekana kumuwania nyota huyo ambaye thamani yake inatajwa kufikia paundi milioni 53.

Wakati vita hiyo ikiendelea kuna ripoti zinadai nyota huyo anaweza kuuzwa pale tu klabu yake ya Juventus itakapompata mbadala wake lakini pia inaelezwa kwa sasa itakuwa rahisi kumpata kuliko kipindi kilichopita ambapo Chelsea ilipeleka ofa nyingi kwa klabu hiyo ili kumvuta nyota huyo.

No comments:

Post a Comment