COURTOIS AKASIRISHWA NA MASHABIKI WA CHELSEA - Darajani 1905

COURTOIS AKASIRISHWA NA MASHABIKI WA CHELSEA

Share This

Nyota wa Chelsea, mlinda mlango Thibaut Courtois amekasirishwa na tabia ya mashabiki wa Chelsea waliofika katika mchezo wa jana ambapo Chelsea ilikuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Leicester city, mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana.

"Ni mbaya kuzomewa na mashabiki wa timu yako haswa pale timu inapohitaji umoja wao kwetu, badala yake wao ndio wanatushambulia kwa kutuzomea. Ni kweli hatukua sawa na bora kama Leicester lakini haikutakiwa kuzomewa" alisema kipa huyo raia wa Ubelgiji ambaye Chelsea inafanya nae mazungumzo ili asaini mkataba mpya, mkataba utakaomfanya apokee mshahara mkubwa kuliko kipa yoyote duniani, paundi 200,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment