MAMBO 3 YA KUYAJUA KUHUSU FRANK LAMPARD - Darajani 1905

MAMBO 3 YA KUYAJUA KUHUSU FRANK LAMPARD

Share This

Nyota wa Chelsea wa zamani ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mchambuzi wa soka, Frank Lampard amekuwa na historia kubwa klabuni Chelsea, akiichezea kwa miaka 13 akisajiliwa klabuni hapo mwaka 2001 akitokea klabuni West Ham mpaka kuja kuondoka Chelsea mwaka 2014 akitajwa na baadhi ya wachambuzi wa soka kuwa ni mmoja kati ya viungo bora kuwai kutokea, akiwa pia ndiye mfungaji bora wa muda wote klabuni Chelsea alipocheza zaidi ya michezo 400 klabuni hapo.

Sasa leo nataka nikuletee mambo matatu muhimu kuhusu nyota huyo

Maisha yake kisoka
"Sikuzaliwa na kipaji kile kikubwa kama ilivyo kwa wachezaji kama Lionel Messi na wengine, ila kufikia hapa nilipo ni kutokana na kupambana na kufanya mazoezi zaidi" alijibu Lampard.

Jambo gumu kulisahau kutokea kwenye maisha yake
"Lilitokea mwaka 2008, ambapo kabla ya siku tatu kuelekea mchezo wa nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya, nilipompoteza mama yangu alipofariki, kocha aliniambia nisicheze mchezo huo ila mi nililazimisha kucheza" alijibu nyota huyo

Umri wake kwa sasa
"Naelekea kutimiza miaka 40 ifikapo mwezi Juni, najivunia maana sasa nna familia na nina furaha pia" alijibu nyota huyo raia wa Uingereza.

Nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi aliwai kuhojiwa ubora wa Lampard akasema "Kumpata mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo na akafunga magoli mengi(kama Lampard) ni jambo adimu sana"

Lakini pia mshambuliaji wa klabu ya Mama site(Man city), Kun Aguero aliwai kuhojiwa akasema "Lampard ni mchezaji bora kwangu maana kwa kiungo kuwa na magoli mengi ni ushujaa"

wewe una lipi unalolikumbuka kwa nyota huyu na gwiji pale klabuni Chelsea?

No comments:

Post a Comment