CHELSEA KUMLETA HAZARD MDOGO - Darajani 1905

CHELSEA KUMLETA HAZARD MDOGO

Share This

Klabu ya Chelsea inaandaa mipango ili kupeleka ofa kwa klabu ya Borrusia Monchnglebach ya nchini Ujerumani inayoshiriki ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga ili kumsajili nyota wa klabu hiyo, Thorgan Hazard ambaye ni mdogo wa nyota wa Chelsea, Eden Hazard.

Chelsea inaandaa mipango hiyo ili kumleta tena nyota huyo ambaye alishawai kusajiliwa kabla na Chelsea mwaka 2012 akitokea Lens ya Ufaransa, kabla ya kupelekwa kwa mkopo Waregem na baadae Borrusia Monchnglebach ambapo huko ndipo alipouzwa kabisa hiyo ikiwa mwaka 2015.

Na sasa Chelsea inatajwa kumtaka tena winga huyo ambaye ni mdogo wa nyota wa Chelsea, Eden Hazard huku akiwa amepitwa miaka 3 na kaka yake huyo ambapo Thorgan kwa sasa ana miaka 24 huku Hazard akiwa ametimiza leo miaka 27.

Lakini dili hilo linatajwa kuanza kufanyika katika dirisha kubwa la usajili.

No comments:

Post a Comment