Nyota mpya wa Chelsea, Ross Barkley ambaye ni raia wa Uingereza ameanza rasmi mazoezi na timu yake hiyo mpya aliyojiunga nayo juzi Ijumaa akisajiliwa kwa dau la paundi milioni 15 akitokea klabuni Everton.
Barkley ameanza mazoezi rasmi ambayo ni mazoezi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea akiwa amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia klabu hiyo ya jijini London huko nchini Uingereza.
"Ni jambo la furaha kwangu, kuichezea timu kubwa kama Chelsea ni jambo la bahati kwangu, napambana kuweza kupona haraka na kuendelezea kipaji changu pale nilipoishia msimu uliopita" alisema Barkley.
Barkley amefanya mazoezi akiwa mchezaji peke yake akijiweka sawa mara baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu uku akisaidiwa na mmoja wa makocha wasaidizi wa kocha Antonio Conte.
Baada ya mazoezi hayo mepesi kwa kiungo huyo mwenye miaka 24 atajiunga rasmi na wenzake na kuanza kufanya mazoezi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea.
No comments:
Post a Comment