UTATOA BEI GANI KWA HAZARD? - Darajani 1905

UTATOA BEI GANI KWA HAZARD?

Share This

Nyota wa Chelsea raia wa Ubelgiji, Eden Hazard amekuwa akifukuziwa na klabu kadhaa duniani huku klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania nayo ikitajwa kwa karibu kumfukuzia nyota huyo anayetimiza miaka 27 leo. Lakini jana wapinzani wa Real Madrid katika ligi kuu nchini umo, Barcelona walikamilisha usajili wa Phillipe Coutinho ambaye amesajiliwa na klabu hiyo kutokea Liverpunga{Liverpool} kwa dau la paundi milioni 142.

Kiasi hicho kimemshangaza nyota wa zamani wa klabu ya Mama site{Man city} ambaye aliwai kulelewa kwenye akademi ya Liverpunga, Joey Barton kuwa usajili huo haukufaa.

Joey Barton ambaye pia ameichezea klabu ya Burnley amesema kwa mchezaji kama Coutinho kusajiliwa kwa kiasi hicho ni kikubwa sana na akalinganisha na je kama kwa Coutinho kasajiliwa kwa kiasi hicho je Eden Hazard wa Chelsea atasajiliwa kwa kiasi gani?

Kupitia mtandao wa Twitter, Barton alituma ujumbe "Nadhani Liverpool inabidi wafurahie sana kwa biashara hii, kumuuza Coutinho kwa kiasi hiki ni biashara nzuri. Hivi kama Coutinho mwenye uwezo wa kawaida unamnunua kwa kiasi kile, je vipi kuhusu Hazard, Kane na Salah? Hazard hana ubora kwa Coutinho, ila Hazard ni zaidi ya bora kwa Coutinho"

***Jambo hilo limenipa maswali kwa Real Madrid ambayo inasema inamtaka Hazard kwa kianzio cha paundi milioni 120, inawezekana ni dharau sana, inabidi watoe ata paundi 200. Hahaaaaa natani, Hazard hapaswi kuuzwa Chelsea maana msaada wake ni mkubwa akiwa na rekodi mpya ya kuhusika kwenye magoli 100 toka asajiliwe mwaka 2012, akifunga magoli 63 na pasi za magoli 37

No comments:

Post a Comment