Ukifika Stamford Bridge, haswa pale Chelsea inapokuwa uwanjani kumenyana na klabu yoyote, pembeni katika majukwaa utaona kuna bango moja limeandikwa "Garden of Eden" likimaanisha Bustani ya Edeni.
Bila shaka nikisema bustani ya Edeni wengi wetu tunaelewa kwamba ilikuwa ni ile bustani aliyokaa mtu wa kwanza kuumbwa na Mungu, Adamu lakini pia akikaa na mwanamama Eva au wengine wanamuitaga Hawa.
Ile bustani ilikuwa na kila kitu kilichoitwa kizuri wanyama na ndege wa kila aina, matunda na kila kila kilichotamanisha kukila. Bila shaka hakuna asiyebisha katika hilo.
Na pale Chelsea kuna binadamu ana kila uzuri wa utamu kama bustani hiyo ya Eden, jina lake linafanana kabisa na hiyo bustani iliyoumbwa na mwenyezi Mungu, ana ufundi na uwezo mkubwa kisoka na hata kuonekana ni kizazi cha dhahabu, anaitwa Eden Michael Hazard.
Ana historia kubwa ndani na nje ya soka, lakini kwa leo acha nimtakie Heri ya kuzaliwa kwake akiwa anatimiza miaka 27.
No comments:
Post a Comment