Nyota mpya klabuni Chelsea raia wa Uingereza, Ross Barkley mwenye miaka 24 ameanza kuifikiria Barcelona mara baada ya kusaini rasmi kuwa mchezaji wa Chelsea hapo juzi siku ya ijumaa.
Barkley akihojiwa kuhusu mchezo huo alisema "Ukiangalia michezo iliyopita, Chelsea ilikuwa inarekodi nzuri ikikutana na Barcelona, ingawa ni mchezo mgumu ila nategemea tutafanya makubwa maana ilikuwa ni ndoto yangu kucheza michuano hii ya klabu bingwa"
Chelsea itamenyana na Barcelona katika hatua ya 16 bora huku nyota huyo mpya aliyesajiliwa kikosini hapo kwa paundi milioni 15 kutokea klabuni Everton, klabu ambayo ameitumikia toka utoto wake.
No comments:
Post a Comment