Chelsea imemaliza mchezo wake wa kombe la FA dhidi ya Norwich katika uwanja wa Carrow road uku matokeo yakiwa 0-0, matokeo ambayo yanamaanisha kurudiana kwa timu hizo ambapo mchezo unaofata utachezwa uwanja wa Stamford Bridge.
Mchezo uliokuwa wa vuta nikuvute huku kipindi cha kwanza kikitumiwa vyema na wenyeji ila wakashindwa kuzigeuza nafasi walizozipata ziwe magoli na hivyo kushuhudia kipindi icho cha dakika 45 za kwanza ziende kwa sare ya 0-0.
Kipindi cha pili kilianza huku Chelsea ikijitahidi kutengeneza nafasi walizozipata ila bahati haikuwa kwao wala kwa Norwich na mpira kuisha kwa sare tasa ya 0-0 huku Willian Borges wa Chelsea akichaguliwa kuwa nyota wa mchezo.
Chelsea itamenyana na Arsenyani katika mchezo unaofata ambapo kocha wa Arsenyani, Arsene Wenger huenda akaukosa mchezo huo kutokana na kupewa adhabu ambapo utachezwa tarehe 10-Januari katika kombe la ligi la Carabao Cup.
No comments:
Post a Comment