NYOTA WA WIKI; HII NDIO SIRI YA HAZARD KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

NYOTA WA WIKI; HII NDIO SIRI YA HAZARD KUTUA CHELSEA

Share This
Nyota wa Chelsea, Eden Hazard amekuwa akitajwa kuhusishwa na klabu kadhaa kumtaka kila baada ya linapofika dirisha la usajili. Amekuwa akitamaniwa na kila klabu kubwa kila pale dirisha la usajili linapofika, hata kabla hajaja Chelsea alipokuwa klabuni Lille huko Ufaransa alitakiwa na vilabu vikubwa kimoja wapo ilikuwa Chelsea. Lakini je unajua siri iliyomfanya nyota huyo atue Chelsea? unajua ilikuwaje mpaka akashawishika kuja Darajani?

Hapa leo nimeamua nikuletee siri kamili iliyomfanya nyota huyo kuachana na klabu nyengine na kutua Chelsea ambapo alitua klabuni hapa mwaka 2012. Nimekuletea siri hii kutokana na kwamba Hazard ndiye nyota wa wiki kwa kipindi hiki mara baada ya kufanya vyema katika mchezo dhidi ya Arsenyani na hivyo kuchaguliwa kuwa mchezaji aliyecheza vyema zaidi kwa upande wa Chelsea.

Ilikuwa mwaka 2012 ambapo nyota huyo alitoka kupata mafanikio makubwa klabuni Lille alishinda tunzo ya mchezaji kinda bora wa ligi kuu Ufaransa maarufu kama Ligue 1 baada ya hapo klabu vigogo za barani Ulaya zikaanza kumfukuzia huku Chelsea ikionekana haina nafasi ya kumpata winga huyo ambapo kwa kipindi icho alikuwa ndio kwanza ana miaka 19.

Siku moja wakati Hazard akiwa mazoezini na klabu yake ya Lille aliitwa na Gervinho na kuambiwa kuna mtu anataka kuongea nawewe kwenye simu, Hazard hakujua ni nani aliepiga kumtafuta ila alipochukua simu alishangaa kusikia aliyetaka kuongea naye alikuwa ni Drogba, alishangazwa na jambo hilo maana kwa kipindiicho Drogba alikuwa mmoja kati ya washambuliaji bora duniani kwa hivyo Hazard alishangaa kwa mtu kama yeye kuongea na mchezaji mkubwa duniani. Ni sawa na tuseme leo mchezaji wa Ndondo Cup hapa Tanzania apigiwe simu na mchezaji yoyote mkubwa Ulaya alafu aambiwe nataka uje huku Ulaya ucheze pamoja namimi, inakuwa ngumu kukataa.

Basi ndicho alichokifanya Drogba na kuanza kumshawishi Hazard, na nyota huyo alikubali kujiunga na Chelsea ingawa mwenyewe aliwai kukiri hakuwai kutamani kuja Chelsea maana Chelsea kwenye ligi kuu haikumaliza katika nafasi nne za juu ambapo hiyo ilimaanisha isingefanikiwa kucheza klabu bingwa Ulaya ila baada ya kubeba taji hilo kule jijini Munich ilipoifunga Bayern Munich ndipo Hazard akaona hakukuwa tena na sababu ya kugoma kujiunga na Chelsea maana ingeweza pia kucheza klabu bingwa kama bingwa mtetezi. Ndipo hapo Hazard akashawishika na kukubali kujiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 35 kutoka klabuni huko Lille.

Siku aliyokamilisha vipimo kupitia mtandao wa Twitter, nyota huyo alituma ujumbe akisema "Nimesaini kwa mabingwa wa Ulaya" kutangaza kuwa sasa ni mchezaji rasmi wa Chelsea.

Leo Hazard amekuwa mchezaji muhimu Chelsea, akiisaidia vyema kutwaa matajikadhaa akiwa chini ya makocha Rafa Benitez, Jose Mourinho, Guus Hiddink na leo yupo chini ya Antonio Conte huku akiwa katikakiwango bora.

No comments:

Post a Comment