Mara baada ya kiungo wa klabu ya Bayern Munich, Arturo Vidal kuhusishwa kutua Chelsea, kocha wa klabu hiyo yenye makazi yake jijini Munich nchini Ujerumani, Jupp Heynkess ameitupilia mbali klabu ya Chelsea juu ya mpango wake wa kumsajili nyota huyo raia wa Chile mwenye miaka 30 kwa sasa.
"Hakuna mawasiliano yoyote kati ya Bayern Munich na Chelsea. Hatuna mpango wa kumuuza Vidal na hata mchezaji yoyote hauzwi haswa katika kipindi hiki" alisema kocha huyo aliyerudishwa Bayern mara baada ya kocha Carlo Ancellotti kutimuliwa klabuni hapo.
Kwa maana hiyo Chelsea inabidi iachane na kiungo huyo ili imtafute nyota mwengine ambapo taarifa hii inaenda kinyume na taarifa zilizosambaa kuwa Chelsea ilishafikia makubaliano na nyota huyo.

KOCHA BAYERN AIPIGA CHINI CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment