HAZARD KUBAKI CHELSEA? NI UAMUZI WA ZIDANE - Darajani 1905

HAZARD KUBAKI CHELSEA? NI UAMUZI WA ZIDANE

Share This
Mara baada ya kuwepo maneno mengi yakimhusisha nyota wa Chellsea, Eden Hazard kutakiwa na klabu ya jiji la Madrid, Real Madrid, kumetoka taarifa kuhusu uhamisho huo unaooonekana kushamiri sana katika dirisha hili la usajili la mwezi januari.

Gazeti moja barani Ulaya limetoa taarifa kuwa usajili wa nyota huyo kutimkia Real Madrid utategemea tu, kama kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane atafukuzwa au kuondoshwa klabuni hapo. Taarifa hiyo inaelezea kiundani kuwa nyota huyo mbelgiji anatakiwa zaidi na kocha Zidane klabuni hapo kuliko anavyotakiwa na mmiliki wa klabu hiyo, Fiorentino Perez.

Zidane amekuwa akivutiwa na Hazard muda mrefu sasa na mara zote amekuwa akiishawishi Madrid imsajili nyota huyo tangu alipoteuliwa kuwa kocha waklabu hiyo ambao ni mabingwa wa dunia wa michuano ya klabu bingwa ya dunia.

Real Madrid mpaka sasa imezidiwa alama 14 na wapinzani wao wakubwa, Barcelona ambapo hiyo inaweza kumfanya kocha huyo akatimuliwa mwezi Juni ambapo itakuwa mwisho wa msimu aambapo kutimuliwa kwake kunaweza kupunguza kasi ya Real Madrid kumfukuzia Hazard.

No comments:

Post a Comment